Thursday, June 12, 2014

Don Jazzy amuajiri mfanyakazi wa Airport alie fukuzwa baada ya kumpa msaada...

Don Jazzy at Tiwa Savage wedding to Tee Billz in Dubai. Photo: Filed

C.E.O wa lebel ya Mavin Don Jazzy amempa ajira mfanyakazi wa  Delta Airline  ambaye amefukuzwa kazi baada ya kumruhusu Don Jazzy kuendesha gari ndogo ambalo hutumika kubebea mizigo ndani ya airport (airport cart) akiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Murtala Mohammed , Lagos,Nigeria.

Mfanyakazi huyo ambaye hajajulikana jina lake amefukuzwa kwa kosa la kumruhusu don Jazzy kuendesha kigari hicho ndani ya uwanja wa ndege  wakati akijua ni kinyume na sheria za ndege hiyo.

Don Jazzy alirekodi video akiendesha kigari hicho wakati akiwa kwenye uwanja huo ndege akisafiri kwenda South Africa kwenye MTV music awards huku mfanyakazi huyo akiwa amekaa pembeni.

Baada ya tukio hilo la kufurahisha, Don Jazzy ameshtuka kusikia mfanyakazi huyo amefukuzwa kazi na kuamua kumuajiri katika label yake ambayo inasimamia kazi za wasanii wakubwa barani afrika kama Tiwa Savage ,Dr Sid na D’banj.

Don Jazzy ameweka wazi Uamuzi wa kumuajiri mfanyakazi huyo kupitia akaunti yake ya instagram na kuambatanisha Video hiyo alirekodi.

“Now dem don fire am. I guess I can post back since he is now my newest employee. I’m sorry bro but welcome to the Mavin Empire. u ll love it here. Osheee. (sic)’...

0 comments: