Monday, June 02, 2014

Taswira ya rais Jomo Kenyatta yaonekana kwenye video mpya ya B.OB 'All I Want'

Rapper wa Marekani B.o.B ameachia video mpya ya wimbo wake aliupa jina la ‘All I want’ ambayo anazungumzia  jinsi ambavyo kwake kitu muhimu zaidi ni kupata pesa.
Katika video hiyo, zimeonekana taswira za pesa za nchi mbalimbali zikiwa zimeunganishwa na nusu taswira ya marais walioko kwenye fedha hizo na taswira ya mtu ambaye anatamani kuwa kwenye noti hiyo.
Katika dakika ya 2 sekunde ya 49 ya video hiyo, inaonekana noti ya Kenya ya shilingi 1000 na nusu taswira ya rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na imeungwa na picha ya mtu ambaye anatamani angekuwa na pesa ama kuwa kweye noti.

0 comments: