Monday, June 16, 2014

Picha:Waandishi wa habari wazua kasheshe kwenye kambi ya timu ya taifa ya Croatia

 
Wachezaji wa timu ya taifa ya Croatia wamegoma kuzungumza na waandishi wa habari waliofika kwenye hoteli ya mjini Bahia ambapo ndipo timu hiyo ilipoweka kambi.Wachezaji wanaotajwa kugoma kuzungumza na vyombo vya habari pamoja na kutoa msimamo wa kambi hiyo ni Dejan Lovren, Darijo Srna, Vedran Corluka na Luka Modric wanao onekana pichani.
Kusudio la wachezaji wa hao kuweka masimamo wa kutozungumza chochote mbele ya vyombo vya habari, limetokana na kuchukizwa na picha zao kuanikwa katika mitandao ambazo zinonyesha wakiwa watupu wakati wakioga hotelini hapo.
 
Hata hivyo mgomo wa wachezaji wa timu ya taifa ya Croatia unakwenda kinyume na taratibu za shirikisho la soka duniani FIFA, ambazo zinatoa ruhusa kwa waandishi wa habari kuzungumza na wachezaji ama kocha pale inapohitajika kwa makusudio maalum.
Katika hatua nyingine kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia, Niko Kovac, ameshangazwa na taarifa hizi kwa kusema, kulikuwa hakuna haja kwa vyombo vya habari kuanika msimamo wao waliouchukua, kwani ilifahamika mapema kosa walilofanyiwa wachezaji wake.
 
Kovac amesema hajaona sababu za vyombo vya habari kuanika hadharani taarifa hizo, kutokana na kambi yake kuwa na utaratibu maalum ambao umewekwa kwa ajili ya kuzungumza na waandishi.
Kikosi cha Croatia kinatarajia kurejea tena uwanjani kucheza mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi la kwanza, ambapo kitapambana na timu ya taifa ya Cameroon hapo kesho huko Arena da AmazĂ´nia, mjini Manaus.
 

0 comments: