Wednesday, November 13, 2013

zifahamu Sigara za kielekitroniki zilizo anza kutumika uingereza , inasemekana zitasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya wavuta sigara

Sigara za kieletroniki , kifaa ambacho kinatumia betri uchochea uvutaji kwa kuchemsha na kufanya kimiminika kilichochanganywa na nikotini kuwa mvuke na mvutaji uvuta mvuke huo badala ya moshi kama ilivyo katika sigara za kawaida . utumiaji wa sigara hizi umekuwa ukiongezeka kwa kasi na kubadilisha utengenezaji wa tumbaku.  Kuwasha sigara ya kielekitroniki kunaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaovuta sigara, hilo limesemwa katika kikao cha kuongeza kifaa hicho kutumiwa na watu wengi zaidi. Japo baadhi ya wataalamu wanaonya kwamba inahitaji ufanyike uchunguzi zaidi juu ya madhara ya kiafya juu ya utumiaji wa sigara hiyo. 
Faida ya sigara ya kielekitroniki ilijadiliwa kwa muda wa siku moja katika mkutano uliowajumuisha wanasayansi 250, watunzi wa sheria, wamiliki wa viwanda na wadau katika jamii ya kifalme mjini London.

0 comments: