Tuesday, April 15, 2014

Kim Kardashian kuanza kulala ndani ya 'kivazi maalumu' ili kutengeneza umbo kwa ajili ya ndoa yake

Kim Kardashian in November, 2013

Mrembo wa kipindi maarufu cha kuonesha maisha halisi The ‘Keeping Up With The Kardashians‘ Kim Kardashian ameanza kujiandaa kwa ajili ya ndoa yake na Kanye ambapo anatarajia kuanza kulala akiwa amevalia ‘kivazi maalamu’cha kutengeneza muonekano mzuri wa umbo lake ..
 
Chanzo cha habari hizi kimeliambia jarida la Grazia kuwa Kim anataka kuoneka vizuri katika siku muhimu katika maisha yake wakati atakapo funga ndoa jiji paris ufaransa mwezi ujao.

Imeelezwa kuwa Kim ambaye ni mama wa mtoto mmoja North, anatarajia kutengeneza muonekano mzuri wa ngozi yake sambamba na kupunguza uzito wakati atakapo kuwa mapumzikoni nchini Thailand na familia yake ..

0 comments: