Tuesday, April 15, 2014

Msanii wa Nigeria ‘Tamiya’ asema elimu sio muhimu kwake!

timaya

Mwimbaji wa Nigeria Timaya ingawa amekiri kuwa elimu ni ufungua wa maisha bora, anaamini Elimu hiyo haipo kwa ajili yake.


Timaya ambaye hakupata elimu ya kutosha amekuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana nchini Nigeria kupitia kazi yake ya muziki
“Elimu sio kwa ajili yangu ,ni muhimu ndio lakini sio kwa ajili yangu.” Ameuambia mtandao wa Thenet.
Ameeleza kuwa alikata tamaa na suala la elimu baada ya kufanya vibaya katika masomo yake wakati akiwa shuleni.
Hata hivyo amewatia moyo wale wanao endelea na masomo na wanahisi wanauwezo wa kufanya vizuri.
“sina ubongo wa kusoma shule lakini kwa wale ambao mnao, tafadhali endeleeni ni vizuri sana.”

0 comments: