Thursday, April 17, 2014

Wizkid na Waje wamtimua manager wao Godwin Tom.

godwin tom sacked wizkid

Wasanii wanaofanya vizuri hivi sasa kutoka Nigeria  Wizkid na Waje wote kwa pamoja wamemfukuza manager wao Godwin Tom kwa kile kinachoelezwa kuwa wametofautina katika kazi.


Imeelezwa kuwa Chanzo cha Godwin Tom kupigwa chini ni kutokana na mabishano makali baina yao yaliotokea siku chache zilizopita kwenye harusi ya mtoto wa aliye wahi kuwa makamu wa rais nchini Nigeria  Atiku Abubakar.

Licha ya kuwa Wizkid na  Waje  wameamua kukaa kimya bila kuzungumza chochote lakini wameliondoa jina la Godwin kwenye kurasa zao za twitter.

 

 kwa upande wa Godwin Tom yeye hajakaa kimya ametoa ya moyoni kupitia  Twitter na Instagram.

“loyal and patient, not stupid on the move and I cant look back ,No regrets at all! Wasted time, I cant get that back so everyday I go hard&When you sleep in a bed of thorns and roses, you learn to adjust, to stay still, to endure hurt and pain, but most important you learn to appreciate a bed without thorns ,there is a difference between giving up and knowing when you have had enough!”

0 comments: