Tuesday, April 29, 2014

Tanzia:mtengenezaji mkongwe wa filamu nchini Nigeria afariki dunia..


 Amaka Igwe (3)

Mtengenezaji mkongwe wa filamu kutoka Nollywood  Nigeria  Amaka Igwe amefariki dunia kutokana na shambulio la asthma akiwa na umri wa miaka 51.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa kampuni yake ya Amaka Igwe studios inasema mwanamama huyo alifariki wakati akikimbizwa hospital baada ya kuzidi.


Mrs Igwe atakumbukwa  kwa kuleta aina mpya ya utengenezaji filamu nchini Nigeria kupitia kampuni yake ya  Amaka Igwe Studios kwa kutengeneza filamu zenye kiwango cha juu na kuwashawishi watengenezaji wengine wa filam nchini humo kufata mfumo wake..
Moja kati ya filamu alizo wahi kuzifanya ni society of watches ,Ladies Vampires pamoja na Tamthilia maarufu nchini Nigeria‘Checkmate’na pia ni muasisi wa kituo cha radio (Top Radio 90.9FM)

0 comments: