Wednesday, April 30, 2014

Mastar waanza kuonesha nia ya kununu timu ya LA Clippers baada ya mmiliki wake kufungiwa..

Diddy, Floyd Mayweather & More Want To Buy The Clippers


Baada ya shirikisho la mpira wa kikapu nchini marekani NBA kumfungia maisha mmiliki wa timu ya LA Clippers Donald sterling kufuatia kupatikana na hatia ya ubaguzi,watu maarufu wameonesha nia ya kuinunua timu hiyo akiwemo Rapper na mfanyabiashara Diddy.


Diddy ameonesha nia ya kutaka kuinunua timu hiyo ya mpira wa kikapu kupitia twetter.
 "I will always be a Knicks fan, but I am a business man. #DiddyBuyTheClippers #NameYourPrice"  alitweet Diddy .

Mtu mwingine alionesha nia ya kutaka kununua timu hiyo ni bondia Floyd Mayweather na muigizaji  Frankie Muniz.
Floyd wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu pambano lake lijalo la masumbwi dhidi ya Marcos Maidana ,amependekeza rafiki zake ambao ni mabillionaire kuweka pesa mezani washindanie kuinunua timu hiyo.
LA Clippers kwasasa inakadiliwa kuwa na dhamani ya  dola million 575..

0 comments: