Monday, September 03, 2012

2FACE IDIBIA ASHUKURU MUNGU KWA KUMUUMBA MWANAMKE…….


Jina lake la kiserikali ni Innocent Idibia…lakini wengu tunamfahamu kama 2face Idibia kutoka pande za Lagos…jiji linalopatikana katika moja ya nchi kubwa barani Afrika upande wa Magharini..Nigeria.
Mwishoni mwa wiki mchizi huyo mkali wa hits kama “African Queen”, “Ole” na “True Love” amefunguka na kuwazungumzia watoto wake na wanawake wote aliozaa nao.
Amesema anapenda kumshukuru MUNGU kwa kumuumba mwanamke kwani kupitia uumbaji wake huo amemuwezesha yeye kupata watoto.
“Watoto ndio dunia yangu, ni mali ghali ambayo nimeweza kumiliki duniani lakini haya yasingewezekana kama MUNGU asingemuumba mwanamke”…amesema 2face.
2face pia ameongeza kwa kusema anawashukuru wanawake wote waliokubali kuzaa nae kwani mpaka sasa ana jumla ya watoto saba na kila mtoto akiwa na mama yake…amesema watoto wake wamekuwa liwazo kwake kila anapokumbwa na matatizo.
Msikilize mwenye hapa……

0 comments: