Tuesday, September 04, 2012

T.I AIZUNGUMZIA “TROUBLE MAN” ALBAM NA UWEZEKANO WA KUFANYA KAZI NA 50 CENT…….


Ni albam ambayo imezungumziwa sana…na inayosubiriwa kwa hamu sana pia..ya jamaa ambaye ni bosi mkubwa wa lebel inaitwa Grand Hustle Records..Crifford Harrison Jr aka T.I inayokwenda kwa jina “Trouble Man” aka “Mtata”.
Now akipiga interview na mtandao wa This Is 50..T.I amezungumzia uwezekano wa kugonga collabo na mtu mzima 50 Cent.
“Hey man..kivyovyote Fifty atakapokuwa tayari..ni kutafuta kitu sahihi kwasababu sote tuna akili ya kufanya vitu kwa usahihi wetu wenyewe..kwa tamaduni na mahali pa watu tunaowawakilisha..tutatafuta kitu kinachozungumza chenyewe na watu”..amesema T.I
“Najaribu kuhakikisha mpaka mwishoni mwa mwaka huu nafanikisha hili…na nitafanya kila namna kuhakikisha kuwa tunafanya kitu kizuri ili kikitoka..kinakuwa classic”..amemaliza T.I
Pia amepata nafasi ya kuzungumzia maono yake katika albam hii na iliyopita na kusema ni kama anaomba msamaha wa kuwa “mtata” (Trouble Man).

0 comments: