Tuesday, January 21, 2014

MTOTO WA FELA KUTI ,SEUN KUTI AMESEMA KUWA MTOTO WA FELA KUMPA STRESS BADALA YA KUMSAIDIA KIMZIKIMtoto wa mkongwe wa muziki barani afrika na muanzilishi wa mtindo wa Afrobeat Fela Anikulapo Kuti , Seun Kuti ameliambia jarida la City People kuwa yeye kuwa mtoto wa fela kuti  haijamsaidia chochote katika kazi zake za muziki.


"siamini kama kuwa mtoto wa Fela Kuti kumenisaidia chochote katika career yangu . ndio mimi ni mtoto wa Fela ,na nimekuwa huku nikipenda muziki kupitia yeye ,wengi wanazani ni rahisi kwa kuwa wapo nje ,kuwa mtoto wa Fela kunanipa Zaidi stress badala ya utajiri “,amesema Suen Kuti

Suen amesema anaamini kama asingekuwa mtoto wa Fala kuti kwa kipaji alicho nacho angekuwa amefika mbali ..’’watu hapa Nigeria wananichukulia tu kama mtoto wa fela kuti lakini hawatizami kiundani nini ninacho kifanya ,sawa mimi ni mtoto wa fela lakini bado inanichukua miaka 10 kupata record deal baada ya kifo chake ‘’ .

Suen amesema anaamini anafanya yake umaarufu na sifa za baba yake hazimsaidii kwa chochote .

0 comments: