Wednesday, January 22, 2014

Rapper Jeezy aingia matatani..

Rapper JEEZY amemakatwa na police kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la police.
Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ ,police wa pande za Georgia walipokea alarm call kutoka kwenye nyumba ambayo girlfriend wa Jeezy anaishi. pOlice walipo fika kwenye nyumba hiyo jeezy mwenye umri wa miaka 36 alianza kuwatolea maneno mabaya police na kushindwa kutoa ushirikiano …

Chanzo cha habari kutoka police kinasema wakati maofficer walipomuuliza nini kilichotokea nyumbani hapo jeezy  aliwajibu “F— you, I ain’t telling you,”
Majibu hayo yaliwafanya police kumkamata na kumshtaki kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano lakini baadae aliaachiwa huru.
hii ni mara ya pili kwa mwaka huu jeezy kukamatwa kwani Jan 3 jamaa alikamatwa kwa kosa la kumpiga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 17 baada ya kutokea mabishano. Lakini Jeezy akajitetea baby mama wake alimuangushia jumba bovu wala hakumpiga mwanae .

0 comments: