Monday, March 31, 2014

Sarkodie awataka wasanii wa ghana kuungana ili walishike soko la muziki afrika..

 
Mkali kutoka Ghana Sarkodie akizungumzia mipango yake kwa mwaka  2014 amesema anataka kuona ghana inateka soko la muziki afrika mwaka huu ,na amepanga  kuwaweka wasanii wakubwa wa ghana katika wimbo mmoja ili kulishika bara zima la afrika .

Sarkodie amesema inaitajika ushirikiano ili kuiweka Ghana kwenye ramani na ni lazima mwaka huu ufanyike wimbo wa pamoja miongoni  mwa wasanii wa kubwa nchini ghana kama Samini, Bandana, R2bees, Castro

Sarkodie  ambaye ni mshindi wa  BET Awards 2012 kupitia kipengele cha “Best International Act Africa” amesema mashabiki wa afrika kusini wanazania yeye ni Mnigeria kutoka na mtizamo kuwa kila msanii anaye fanya vizuri anatoka Nigeria, sasa ili ghana ifanya vizuri ni lazima kushirikiana mmoja mmoja haiwezekani


0 comments: