R&B diva Alicia Keys amekumbwa
na msala wa kesi inayohusiana na kuvunja sheria ya hakimiliki, yaani copyright
infringement kwa kunakili bila ruhusa ya mmiliki baadhi ya mistari inayosikika
kwenye wimbo wake akiwa na Nicki Minaj ‘Girl on Fire’.
Keys anashtakiwa na mwandishi wa
nyimbo anaeitwa Earl Shuman ambae anadai kuwa Alicia Keys aliiba mistari miwili
kwenye wimbo unaoitwa “Lonely Boy” ambao aliandika akishirikiana na mwanamuziki
Leon Carr na kurekodiwa na Eddie Holman kwa jina la “Hey There Lonely Girl”
mwaka 1970 na ikashika nafasi ya pili kwenye Billboard chats enzi hizo.
Kwa mujibu wa blog ya blogger
maarufu Friedman, Alicia Keys alitumia sekunde mbili tu za kwenye wimbo halisi
aliokopi lakini ndizo zilizomsaidia kurekodi wimbo wake mzima wa ‘Girl on
Fire.’
Mwandishi huyo mkongwe katika sanaa
ya uandishi wa nyimbo ambao kwa wenzetu walioendelea wanauheshimu sana ametoa
ripoti kupitia blog ya Friedman (show bizz 411) kuwa ameshafungua kesi mahakamani
akimshtaki Alicia Keys, kampuni ya Sony Music waandishi Salaam Remi na Billy
Kravan ambao wamehusika pia kuandika “Girl On Fire”. Katika mashtaka hayo
Shuman ameeleza kuwa mshitakiwa(Alicia Keys) amevunja sheria kwa kuingilia hakimiliki
yake kwa hiyo anahitaji fidia ya kazi yake, ikiwa ni pamoja na faida
iliyopatikana kwenye wimbo huo “Girl on Fire.”
Wakati mrembo huyo anahitajika
kujibu mashtaka mahakamani, yeye anaendeleza mashambulizi ya kuumaliza mwaka na
vitu vikali na ameachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa “Brand New Me” ambayo
iko kwenye album yake ya “Girl on Fire”
Haya mambo yangekuwa yana exist hapa
kwetu nadhani kuna wasanii wengi sana wangekuwa wanapishana mahakamani
sababu iko list ndefu sana, na kazi za watu wengine zingeheshimiwa.
0 comments:
Post a Comment