Monday, December 24, 2012

RIHANNA AICHANGIA HOSPITAL YA KWAO BARBADOS DOLA 1.75 MIL ILI KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KANSA…..


Baaada ya mafanikio ambayo bado anaendelea kuyapata siku hadi siku…Rihanna aichangia kiasi cha dola 1.75 milioni hospitali ya huko kwao Barbados.
E! News imeripoti kuwa R&B Diva Rihanna ametoka kiasi hicho kama kumbukumbu ya marehemu bibi yake Clara “Dolly” Braithwaite ambaye alifariki kutokana na kansa mwezi June mwaka huu. 
Mchango huo umeelekezwa kwenye idara ya ‘rediotherapy’ katika hospitali ya Queen Elizabeth iliyoko Bridgetown huko Barbados na hiyo idara inatakiwa iitwe ‘Clara Braithwaite Centre for Oncology and Nuclear Medicine’
“Hii ni njia yangu ya kurudisha Barbados..kwa namna ya ‘philanthropy’..kwa kusaidia muendelezo wa mpango huu wa kisasa…na naamini hii itakuwa na faida kubwa sana kwa watu wa Barbados…itaokoa maisha na kuwafanya waishi muda mrefu zaidi”….amesema Rihanna.

0 comments: