Wednesday, December 19, 2012

T.I ASEMA..JAY Z ALITAKIWA AWEMO KWENYE “TROUBLE MAN: HEAVY IS THE HEAD”……..

 

Baada ya kucheleweshwa kwa miezi kadhaa…mzigo wa mtu mzima T.I “Trouble Man: Heavy is the Head” hatimaye uko kitaa hivi sasa…akipiga interview na XXL Magazine…mfalme huyu toka South anayemiliki lebel ya Grand Hustle Records amezungumzia collabo ambayo aliipanga iwemo lakini alishindwa kuikamilisha kwenye mzigo wake huu wa nane.

Kwa mujibu wa T.I mwenyewe ni kwamba mtu mzima Jay Z alitakiwa aingie kwenye mkono unaitwa “G Season” lakini ikashindikana na badala yake akaingia bwana mdogo aliye chini ya MMG…Meek Mill na kuweka verse kwenye beat ya ngoma hiyo iliyotengenezwa na Cardiak.

“Nilimuomba Jay Z aingie kwenye ngoma hiyo…najua jamaa yuko tyt sana na mambo kibao anayoyafanya…na baada ya kushindikana nikamkamata Meek Mill…tulikuwa kwenye shughuli flani hivi ya Kanye West…nikamwambia…’mwana kuna kazi moja naomba unisaidie’..tukatoka tukaenda sehemu tukapata msosi then tukadondoka kwa studio ya Just Blaze huko Harlem na tukamaliza mzigo.”…amemaliza mtu mzima T.I.

0 comments: