Na Denis Mlowe – Iringa
Muziki wa kizazi kipya
wengi wanaujua kama bongo fleva wazidi kuwavutia viongozi mbalimbali na wengine
wanaimba hadi sasa kama Joseph Mbilinyi aka Sugu, Vick Kamata sasa amejitokeza
mbunge mwengine wa viti maalum toka chama cha mapinduzi Ritta Kabati na
kuufanya uwe gumzo katika maisha ya watanzania na nchi za jirani kitu
kinachofanya watu mbalimbali kujitokeza kuupenda na wengine kuamua kuingia kwa
kasi katika tasnia hii ya burudani Tanzania.
Katika kuukuza zaidi
muziki huu Mbunge wa Viti maalum kupita chama cha Mapinduzi mkoani Iringa Ritta
Kabati akishirikiana na wasanii chipukizi 20 wa kwanza waliotokana na shindano
la kutafuta vipaji la Kabati Katiba Star Search amefanikiwa kutoka wimbo mmoja
unaokwenda kwa jina la 'Iringa Bila Ukimwi Inawezakana' uliofanywa katika
studio za Top Magic Sound chini ya mzalishaji anayekuja kwa kasi pande za
Nyanda za juu Kusini Ecko Msigwa.
Wimbo huo ni harakati
za mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga kama
uvutaji wa bangi, kuepukana na maambukizi ya ukimwi katika mkoa huu ambao
unaongoza kwa sasa nchini Tanzania na amesema kwamba wakati anafikiria kuingiza
mashairi hayo kwa kweli alikuwa katika hali ya huzini kwa jinsi vijana
walivyoweza kufanya vizuri katika wimbo huo kwa lengo la kuwakomboa watanzania
kupitia muziki.
Baadhi ya mashairi ya
hayo ni ‘ndugu zangu watanzania nina maumivu makali sana, tumepoteza ndugu
zetu, jamaa zetu na marafiki zetu dira ya maendeleo inateketea ni wakati wetu
kupambana iringa bila ukimwi inawezekana’ “ kwa kweli nina uhakika wa
kuwafunika vijana hawa katika wimbo huu ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na
wakazi wa mkoa huu kwa kuwa ni mkusanyiko wa vipaji vya kweli vilivyotokana na
shindano nililoandaa” alisema Kabati
Wimbo huo unatarajia
kuzinduliwa rasmi leo katika radio zote za Nyanda za Juu Kusini na kisha
kusambazwa katika radio zote nchini Tanzania na amewataka wadau kuwapa nguvu
vipaji hivi kwa kununua kazi za vijana kwa lengo la kuwaongeza kipato na
kuondoka na maisha ya vijiweni.
@kwa hisani ya francisgodwin.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment