Friday, December 21, 2012

“NIGGAZ IN PARIS” YA JAY Z NA KANYE WEST YATAWAZWA TRIPLE PLATINUM…

Ni mwaka tayari umekatika tangu Kanye West na Jay Z waiachie kitaani albam yao ya pamoja…”Watch The Throne”…albam ambayo mpaka hivi sasa imeshanyakuwa tuzo kibao sana…ambayo kadri muda unavyozidi kusonga ndivyo tracks ndani ya mzigo zinavyozidi kushika zaidi.
Kwa mujibu wa HHNM…”Niggaz in Paris” moja kati ya ngoma makini sana zinazopatikana kwenye albam hiyo tayari imetawazwa triple platinum baada ya kufikisha mauzo ya nakala milioni 3.
Mafanikio ya baadhi ya ngoma kutoka ndani ya albam hiyo hayajaishia hapo coz ngoma “No Church in the Wild” ambayo Frank Ocean amenyonga choras flani matata pia imetawazwa GOLD..tayari imekuwa ikitumika kwenye matangazo ya magari, movies na bidhaa zingine kibao.
“Niggaz in Paris” ni ngoma Jay Z na Kanye wanaitegemea sana kwenye kuamsha watu mara zote wanapokuwa kwenye concerts mbalimbali…na mara nyingi wamekuwa wakii-perform zaidi ya mara saba kwenye tamasha moja kutokana na maombi ya fans...


0 comments: