Friday, December 28, 2012

SWAHILI RAP INSPIRATION BY THE NEW AGE - By Ezden “The Rocker”

 Hip Hop ni utamaduni ulioanzishwa na jamii ya wamarekani weusi huko Bronx, New York City miaka ya sabini (1970's) Na mara nyingi neno hili limekua liktumiwa kumaanisha Muziki wa Rap lakini katika uwanja mpana zaidi HipHop kwa ujumla inaundwa na nguzo kama 1. Break dancing 2. Rapping 3. Graffiti art 4. DJing 5. Beatboxing 6. Street fashion 7. Street Language 8. Street Knowledge 9. Street Entrepreneurialism.
Kwa kuangalia kipengele ambacho ndio 'common' sana RAPPING/ Hip Hop Music jamii imekua na uelewa mkubwa sana ktk hili baada ya kupata mashabiki wengi duniani na kua na influnce kwa watu wengi pia kama wasanii (Rappers) toka mataifa mbali mbali.
Hapa Bongo tumekua tukiona wasanii wengi wa Hip hop tangu enzi za Kwanza Unit, kwa uchache tu kuja mpaka kina Mr. Two (Sugu), Prof. Jay (Wa kipindi wa kile), Fid Q (Ambae anaendelea ku-inspire wasanii wengi sana mpaka leo), Jay MO, Hashim Dogo na wengine wengi waliofanya HipHop ya kweli.
Muda wote huo tumekua tuki-experience mabadiliko katika uandishi wa mashairi na Flow tofauti tofauti mpaka kwa wasanii kama Joh Makini, Izzo B, Geez Mabovu, Watengwa, Nako 2 Nako Soldiers na wengine kibao walioonyesha wazi kua block hii imeendelea kuwa na mabadiliko mengi tu mpaka kutokea kwa mtindo Fulani mpya wa kufanya muziki wa Rap maarufu kama "New Era Hip hop".
NEW ERA HIPHOP imekuja na majina kama Nikki Mbishi, Stereo, One The Incredible na badae kidogo watu kama Songa, Ghetto Ambassodor, P The Mc, Philly Teknics, Zaiid, Shashow, Nash Emcee, Azma, Kad Go, Young Killah na wengine wengi ambao wameonyesha kama Hip Hop inataka kuchukua chanel nyingine au kua na aina fulani ya Rap ambayo imekua ikienda sambamba sana na uwezo mkubwa wa ufanyaji wa Mitindo huru yaani Freestyles.

Kitu ambacho mpaka sasa kinaleta maswali mengi ni kwamba ubunifu kwa sasa umekwenda wapi hususani kwa Emcee's wapya sababu sehemu kubwa ya wanaotokea inakua kama tayari wamekua inspired na wakina NIKKI MBISHI, STEREO na ONE, Emcee's ambao hawana historia ndefu sana kwenye ramani ya Hip Hop lakini wamefanikiwa kuwa na ushawishi kwa nguvu kubwa mpaka wasanii wengi wa leo wanataka kuwa na style kama zao hali kadhalika uandishi.
Binafsi nimejaribu kuangalia kwa ukaribu na kugundua kua ni kujituma, kua wabunifu zaidi na kutoangalia sana soko bali kuifanya HipHop kama utamaduni ndio kumeleta ladha Fulani mpya ambayo sasa kila Emcee mpya anataka kufanya kama hawa wachache.
Katika kujaribu kuliangalia suala hili kwa mtazamo mwingine nimeona sio mbaya kupata mawazo ya hawa wahusika ambao wamekua kama kioo kwa Ma-Emcee wengi wapya, nikianza na STEREO anasema “ Nafarijika sana kuona Ma-Emcee wanajaribu kufanya HipHop kama mimi ninavyofanya au kua hapa nilipo”.
STEREO anaendelea kusema, “Cha msingi wasiache pia kuwsikiliza Ma Emcee wengine wakali wa HipHop kwa hapa Tanzania na nje ya nchi kwa mfano SEAN PRICE, FID Q, SONGA, GHETTO AMBASSADOR, P THE MC, NASH EMCEE, ZAIID, NIKKI WA PILI, EDO G, MASTER ACE n.k. Pia wawe na tabia ya kujifunza mambo mengi wasiyoyafahamu na kujua kinachojiri duniani kila siku iendayo kwa Mwenyezi Mungu”
Stereo anamaliza hivyo pamoja na ku-share baadhi ya wasanii ambao wanaendelea kumu-inspire yeye. Wakati NIKKI MBISHI akifunguka kwa kingereza na kusema, “I think Kids had to look for perfect, influential and inspirational cats to make them up, so they decided to put us into consideration for they’ve realized our skillz, tactics and efforts we all applied to be great, also we didn’t commercialize but we modernized the game through old skool and new skool rap basis”.
Katika kushauri Emcees wengi MBISHI anasema,”My advice, Emcees should always be fast learning students by stopping thinking that they’ve made it!”
NIKKI MBISHI akimaliza kwa kuonyesha njia sahihi inayoweza kutumiwa na Emcees wengi wapya ili kufanikiwa au kufika wao walipo.
Kila mtu anakua na inspirations zake, role models na vitu kama hivyo lakini mwisho wa siku ni juhudi zako katika kuhakikisha unafikia lengo na kujituma zaidi katika fani hiyo, kuiga au kuchukua style ya mtu sio mbaya lakini wanasema iga halafu boresha ili ipatikane style mpya atakayo kupa nafasi katika uwanja huu wa fani ya Rap.
For comments: ezdy2010@gmail.com
Mobile; +255 716 113380
Twitter: Follow me @ezdenhiphop
www.facebook.com/ezden

0 comments: