Monday, December 24, 2012

DRAKE AMUOMBA JAJI KUTUPILIA MBALI SHAURI LA KESI YA KUPIGANA CHUPA CLUB NA CHRIS BROWN…..


Japokuwa yeye mwenye Drake alikuwepo….na inawezekana akawa ni sehemu ya kilichotokea kwenye ugonvi ndani ya nightclub baina yake na Chris Brown…lakini anaamini ahusiki na muonekano mbaya wa W.i.P. nightclub kwa jamii kwa sasa.
TMZ imeripoti kuwa Drake amemuomba jaji alitupilie mbali shauri hilo hata kama urushwaji wa chupa ulianza baada ya Drizzy na Chris Brown walianza kurushiana chupa.
Na katika kukandamizia hilo Drake amesema hata ‘New York Times’ magazine limeandika kuwa club hiyo imekuwa na historia ya fujo na matatizo mengine.
Club hiyo ‘W.i.P. Nightclub’ ilifungwa mwaka 2011 na NYPD (mamlaka) na siku za nyuma ilishawahi kusimamishiwa kibali chake kutokana na matukio ya fujo kufululiza kwa muda mrefu.
Nyakati fulani Chris Brown aktika moja ya interviews zake aliwahi kukataa kuizungumzia ishu hiyo kwa sababu tayari ilikuwa kwenye vyombo vya kisheria…

0 comments: