Friday, December 21, 2012

T.I AZUNGUMZIA ALIVYOM’SIGN MEEK MILL GRAND HUSTLE….NI SEHEMU YA SAFARI YA MEEK MILL KIMUZIKI….Kabla hajawa rapper anayefahamika sana kama ilivyo sasa chini ya Maybach Music lebel…mtu mzima Meek Mill alikuwa amesign kwa muda mfupi na Grand Hustle Records ya T.I.
Akipiga interview na Power 99 fm ya Philadelphia..bosi wa zamani wa rapper huyo na mfalme kutoka South..mtu mzima T.I amezungumzia mwanzo wa Meek Mill pale Grand Hustle.
Tip amesema bado anahisi kubeba majuto ya haja kwa kumwachia Meek Mill aondoke…lakini pamoja na hayo yote anajivunia mafaniko ya mchizi huyo kwa sasa akiwa na lebel nyingine.
“Mimi na Meek Mill tulikuwa pamoja awali Grand Hustle..kutokana na mambo ya hapa na pale yaliyokuwa yananizunguka kwa wakati ule sikuweza kufanya chochote kwa yeyote…na ndicho kilichomfanya aondoke na kwenda kwa Rozay…japo nilikuwa na mkataba naye lakini sikuona maana ya mimi kumzuia wakati sikuwa na uwezo wa ku’match na situation yake…bado nilikuwa hata nikirudi nyumbani ninakuwa mambo mengi sana ya kufanya…so kama uamuzi wa kwenda MMG ulikuwa ni uamuzi mzuri kwake sikuona namna ya kulizuia hilo”…amesema T.I
Akaongeza..”Ninafurahia mafanikio yake…kiukweli kabisa…na najisikia kama nami ningehusika kwenye mafanikio hayo ingekuwa mzuka sana…mwisho wa siku maisha ndivyo yalivyo…wakati mwingine hakitokei kile unachotaka kitokee”.

0 comments: