Friday, December 28, 2012

SWAHILI RAP INSPIRATION BY THE NEW AGE - By Ezden “The Rocker”

0 comments

 Hip Hop ni utamaduni ulioanzishwa na jamii ya wamarekani weusi huko Bronx, New York City miaka ya sabini (1970's) Na mara nyingi neno hili limekua liktumiwa kumaanisha Muziki wa Rap lakini katika uwanja mpana zaidi HipHop kwa ujumla inaundwa na nguzo kama 1. Break dancing 2. Rapping 3. Graffiti art 4. DJing 5. Beatboxing 6. Street fashion 7. Street Language 8. Street Knowledge 9. Street Entrepreneurialism.
Kwa kuangalia kipengele ambacho ndio 'common' sana RAPPING/ Hip Hop Music jamii imekua na uelewa mkubwa sana ktk hili baada ya kupata mashabiki wengi duniani na kua na influnce kwa watu wengi pia kama wasanii (Rappers) toka mataifa mbali mbali.
Hapa Bongo tumekua tukiona wasanii wengi wa Hip hop tangu enzi za Kwanza Unit, kwa uchache tu kuja mpaka kina Mr. Two (Sugu), Prof. Jay (Wa kipindi wa kile), Fid Q (Ambae anaendelea ku-inspire wasanii wengi sana mpaka leo), Jay MO, Hashim Dogo na wengine wengi waliofanya HipHop ya kweli.
Muda wote huo tumekua tuki-experience mabadiliko katika uandishi wa mashairi na Flow tofauti tofauti mpaka kwa wasanii kama Joh Makini, Izzo B, Geez Mabovu, Watengwa, Nako 2 Nako Soldiers na wengine kibao walioonyesha wazi kua block hii imeendelea kuwa na mabadiliko mengi tu mpaka kutokea kwa mtindo Fulani mpya wa kufanya muziki wa Rap maarufu kama "New Era Hip hop".
NEW ERA HIPHOP imekuja na majina kama Nikki Mbishi, Stereo, One The Incredible na badae kidogo watu kama Songa, Ghetto Ambassodor, P The Mc, Philly Teknics, Zaiid, Shashow, Nash Emcee, Azma, Kad Go, Young Killah na wengine wengi ambao wameonyesha kama Hip Hop inataka kuchukua chanel nyingine au kua na aina fulani ya Rap ambayo imekua ikienda sambamba sana na uwezo mkubwa wa ufanyaji wa Mitindo huru yaani Freestyles.

Kitu ambacho mpaka sasa kinaleta maswali mengi ni kwamba ubunifu kwa sasa umekwenda wapi hususani kwa Emcee's wapya sababu sehemu kubwa ya wanaotokea inakua kama tayari wamekua inspired na wakina NIKKI MBISHI, STEREO na ONE, Emcee's ambao hawana historia ndefu sana kwenye ramani ya Hip Hop lakini wamefanikiwa kuwa na ushawishi kwa nguvu kubwa mpaka wasanii wengi wa leo wanataka kuwa na style kama zao hali kadhalika uandishi.
Binafsi nimejaribu kuangalia kwa ukaribu na kugundua kua ni kujituma, kua wabunifu zaidi na kutoangalia sana soko bali kuifanya HipHop kama utamaduni ndio kumeleta ladha Fulani mpya ambayo sasa kila Emcee mpya anataka kufanya kama hawa wachache.
Katika kujaribu kuliangalia suala hili kwa mtazamo mwingine nimeona sio mbaya kupata mawazo ya hawa wahusika ambao wamekua kama kioo kwa Ma-Emcee wengi wapya, nikianza na STEREO anasema “ Nafarijika sana kuona Ma-Emcee wanajaribu kufanya HipHop kama mimi ninavyofanya au kua hapa nilipo”.
STEREO anaendelea kusema, “Cha msingi wasiache pia kuwsikiliza Ma Emcee wengine wakali wa HipHop kwa hapa Tanzania na nje ya nchi kwa mfano SEAN PRICE, FID Q, SONGA, GHETTO AMBASSADOR, P THE MC, NASH EMCEE, ZAIID, NIKKI WA PILI, EDO G, MASTER ACE n.k. Pia wawe na tabia ya kujifunza mambo mengi wasiyoyafahamu na kujua kinachojiri duniani kila siku iendayo kwa Mwenyezi Mungu”
Stereo anamaliza hivyo pamoja na ku-share baadhi ya wasanii ambao wanaendelea kumu-inspire yeye. Wakati NIKKI MBISHI akifunguka kwa kingereza na kusema, “I think Kids had to look for perfect, influential and inspirational cats to make them up, so they decided to put us into consideration for they’ve realized our skillz, tactics and efforts we all applied to be great, also we didn’t commercialize but we modernized the game through old skool and new skool rap basis”.
Katika kushauri Emcees wengi MBISHI anasema,”My advice, Emcees should always be fast learning students by stopping thinking that they’ve made it!”
NIKKI MBISHI akimaliza kwa kuonyesha njia sahihi inayoweza kutumiwa na Emcees wengi wapya ili kufanikiwa au kufika wao walipo.
Kila mtu anakua na inspirations zake, role models na vitu kama hivyo lakini mwisho wa siku ni juhudi zako katika kuhakikisha unafikia lengo na kujituma zaidi katika fani hiyo, kuiga au kuchukua style ya mtu sio mbaya lakini wanasema iga halafu boresha ili ipatikane style mpya atakayo kupa nafasi katika uwanja huu wa fani ya Rap.
For comments: ezdy2010@gmail.com
Mobile; +255 716 113380
Twitter: Follow me @ezdenhiphop
www.facebook.com/ezden

ALICHOANDIKA D KNOB # KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK......

0 comments

Thursday, December 27, 2012

KAZI IMEANZA….ILE RAP BATTLE YA CASSIDY NA MEEK MILL….HII NI KARATA YA KWANZA YA MEEK MILL…

0 comments

Vita kati ya marapper wawili, Cassidy na Meek Mill wa Maybach tayari imeanza rasmi.
Baada ya juzi kati tu kujibizana kwenye twitter na kukubaliana kuingia kwenye rap battle…na hiyo ni baada ya mtu mzima Cassidy kuachia a diss track kwa Meek Mill “Me, Myself & iPhone”..sasa Meek Mill leo ameachia track yake ya kwanza kama diss kwa mtu mzima Cassidy.
Track inaitwa “Repo”….track ambayo Meek Mill amekwenda straight sana kwa mchizi bila kupindisha maneno na kuweka wazi changamoto anazokutana nazo kwenye game kutoka kwa marapper wa muda mrefu kidogo kama Cassidy…kwenye ngoma kuna lines anasema..” You talkin' 'bout a battle rap? How you gon' handle that? / Hundred grand pussy nigga? You ain't got the time for that / You ain't got the stacks for that / You know what we laughin' at," 
 baaada ya hiyo picha ilioambatana na diss track ,cassady ali-tweet maneno haya ,,

Sikiliza track hiyo hapa......... 

Chris Brown anajua kuwapanga Karuache Tran na Rihanna! Baada ya kula bata na Karuache kule Paris,Christmas hii alikuwa na Rihanna Los Angeles...

0 comments

Pamoja na kwamba mpaka sasa Chris Brown na Rihanna hawakubali  kuwa wao ni couples lakini matukio ya kuthibitisha hili yanazidi kuonekana.
Jana (december 25) katika kusheherekea sikukuu ya Christmas star kutoka Barbados Rihanna mwenye miaka 24 aliamua kuchukua flight hadi Los Angeles ambako ali-join na Chris Brown kushuhudia mechi ya mpira wa kikapu baina ya Lakers na Knicks iliyopigwa katika uwanja wa Staples Center, Los Angeles  Marekani.
Ni kama wametoa picha yenye maelezo kuwa wameamua kurudiana tena na kuendelea na maisha yao pamoja, na hii ni baada ya Chris Brown kuonekana kuvuruga makubaliano yao hivi karibuni na kula bata na mpenzi wake wa zamani Karuache Tran huko Paris Ufaransa, kitu ambacho kilimkera sana Rihanna na kuandika tweet za matusi ambazo zilionekana kabisa kuwa zilielekezwa kwa Chris Breezy kwa kukutana tena na Karrueche Tran wakati huo Rihanna yuko mpweke kwenye mapumziko yake akitegemea ujio wa Chris Brown.
Chris Brown na RiRi walionekana wenye furaha sana wakitabasamu na kucheka mara kwa mara wakati wanaangalia mechi ya Lakers siku hiyo ya Christmas huko Los Angeles. Ni kama Chris Brown anaweza kuwamudu na kuwacontrol warembo hawa wawili matata.

Baada ya game kuisha RiRi alitweet picha aliyopiga na Chris Brown wakiwa wamepose katika Porshe 911 Turbo S aliyozawadiwa na lebel yake ya Roc Nation ya mtu mzima Jay Z hivi karibuni, na picha hiyo ilikuwa na caption iliyosomeka "Thug Life, Merry Christmas".
 
 
 


 
 

DAN ROCK FEAT. AT - KITOLA OFFICIAL VIDEO FULL HD

0 comments
Official Video ya msanii DAN ROCK feat. AT. Nyimbo inaitwa KITOLA na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri

Wednesday, December 26, 2012

WIZ KHALIFA NA 50 CENT KUFANYA MOVIE PAMOJA....

0 comments

Baada kutoka na film ya Mac & Devin Go To High School akiwa na  Snoop Dogg ,Wiz Khalifa amenogewa na biashara hiyo na sasa yupo kwenye mipango ya kutengeneza movie nyingine ambayo itamshirikisha star wa rap ,
Akipiga story na DJ Whoo Kid ,wiz amedhibitisha kuwa  alizungumza na 50 Cent juu ya kufanya  movie na soundtrack pamoja , “ nilikuwa na 50 Vegas na tukazungumza juu ya kutengeza movie na soundtrack pamoja . “nataka niwe drug dealer kwenye hiyo movie. Nataka nishike pistol. Akatania ,Nataka niwashoot ,”
Check out interview yake na DJ Whoo Kid , Wiz anazungumzia ujauzito alionao Amber Rose, na kwanini snoop or Curren$y hawajatokelezea kwenye albam yake, na anasubiri kufanya kazi Dr. Dre, 

Tuesday, December 25, 2012

MBWANA SAMMATA ...AOMBA MSAMAHA #KUPITIA FACEBOOK , ..

0 comments


TAARIFA KUTOKA JWTZ: WATAMCHUKULIA HATUA KALI MWANAJESHI ALIEPIGA PICHA NA LEMA,

0 comments
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwa katika gazeti la Mwanandhi la Desemba 24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.

Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.

Ilikuwa rahisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu

Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga
 source:http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/373747-tamko-la-jwtz-juu-ya-picha-ya-lema-na-mwanajeshi-katika-mwananchi-la-leo.html



Monday, December 24, 2012

RIHANNA AICHANGIA HOSPITAL YA KWAO BARBADOS DOLA 1.75 MIL ILI KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KANSA…..

0 comments

Baaada ya mafanikio ambayo bado anaendelea kuyapata siku hadi siku…Rihanna aichangia kiasi cha dola 1.75 milioni hospitali ya huko kwao Barbados.
E! News imeripoti kuwa R&B Diva Rihanna ametoka kiasi hicho kama kumbukumbu ya marehemu bibi yake Clara “Dolly” Braithwaite ambaye alifariki kutokana na kansa mwezi June mwaka huu. 
Mchango huo umeelekezwa kwenye idara ya ‘rediotherapy’ katika hospitali ya Queen Elizabeth iliyoko Bridgetown huko Barbados na hiyo idara inatakiwa iitwe ‘Clara Braithwaite Centre for Oncology and Nuclear Medicine’
“Hii ni njia yangu ya kurudisha Barbados..kwa namna ya ‘philanthropy’..kwa kusaidia muendelezo wa mpango huu wa kisasa…na naamini hii itakuwa na faida kubwa sana kwa watu wa Barbados…itaokoa maisha na kuwafanya waishi muda mrefu zaidi”….amesema Rihanna.

DRAKE AMUOMBA JAJI KUTUPILIA MBALI SHAURI LA KESI YA KUPIGANA CHUPA CLUB NA CHRIS BROWN…..

0 comments

Japokuwa yeye mwenye Drake alikuwepo….na inawezekana akawa ni sehemu ya kilichotokea kwenye ugonvi ndani ya nightclub baina yake na Chris Brown…lakini anaamini ahusiki na muonekano mbaya wa W.i.P. nightclub kwa jamii kwa sasa.
TMZ imeripoti kuwa Drake amemuomba jaji alitupilie mbali shauri hilo hata kama urushwaji wa chupa ulianza baada ya Drizzy na Chris Brown walianza kurushiana chupa.
Na katika kukandamizia hilo Drake amesema hata ‘New York Times’ magazine limeandika kuwa club hiyo imekuwa na historia ya fujo na matatizo mengine.
Club hiyo ‘W.i.P. Nightclub’ ilifungwa mwaka 2011 na NYPD (mamlaka) na siku za nyuma ilishawahi kusimamishiwa kibali chake kutokana na matukio ya fujo kufululiza kwa muda mrefu.
Nyakati fulani Chris Brown aktika moja ya interviews zake aliwahi kukataa kuizungumzia ishu hiyo kwa sababu tayari ilikuwa kwenye vyombo vya kisheria…

Saturday, December 22, 2012

RAPPER FAT JOE HUENDA AKAENDA JELA MIAKA MIWILI KWA KUKWEPA KULIPA KODI...

0 comments
Rapper Fat Joe ameshitakiwa na serikali ya marekani kwa kosa la kukwepa kulipa kodi,
Fat Joe au Joseph Cartagena mwenye umri wa miaka 42 anafahamika kwa kazi alizowahi kuzifanya late Big Pun, Terror Squad na wakali wengine kibao, amepatishwa kizimbani katika mahakama ya New Jersey,na uhenda akashitakiwa miaka miwili jela lakini kwasasa yupo nje kwa dhamani ya $250,000,
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa  April mwakani .

Friday, December 21, 2012

LULU AACHIWA KWA DHAMANA

0 comments
Na Prince Akbar
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo asubuhi imemuachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayetuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ baada ya kupitia vifungu vya sheria.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kubadilisha mashitaka ya mwanadada huyo kutoka kesi ya mauaji hadi kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, hata kama atashindwa kesi, Lulu hatapewa hukumu ya kunyongwa kwa kuwa anatuhumiwa kwa kesi ya kuua bila kukusudia na kwa mujibu wa kifungu cha sheria, anaweza kufungwa maisha au miaka kadhaa.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam.
Lulu aliyecheza filamu kadhaa na marehemu Kanumba waliyeibuka naye katika kundi la Kaole, Magomeni, anadaiwa alimsukuma Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican, ambaye pia inadaiwa alikuwa mpenzi wake.
Inaelezwa baada ya tukio hilo, Lulu alikimbia nyumbani kwa Kanumba na mdogo wa The Great, Sethi Bosco akaenda kuchukua gari kumpeleka kaka yake hospitali ya Muhimbili, ambako alipofika iligundulika amekwishafariki dunia.
Sethi alikaririwa akisema kwamba siku ya tukio, Lulu alikwenda kwao usiku wa manane na alipofika yeye (Sethi) alimuacha aongee na kaka yake. Sethi alidai aliwaacha sebuleni akaingia chumbani kwake na baadaye akasikia wameingia chumbani (kwa Kanumba).
Sethi alisema baada ya muda alisikia kelele za dalili ya ugomvi na baada ya muda Lulu alitoka kumwambia (Sethi) juu ya hali ya Kanumba kubadilika na kuwa mbaya.
Sethi alidai aliposikia hivyo akashituka na kwenda chumbani ambako alimkuta kaka yake katika hali mbaya, povu likimtoka mdomoni hivyo kuchukua hatua ya kumuita daktari wake, kabla ya kumkimbiza Muhimbili.
Lulu alikamatwa asubuhi ya kuamkia siku ya tukio hilo, linalodaiwa kutokea usiku wa manane na kuwekwa kizuizini katika kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam, kabla ya kufikishwa mahakamani.
Uchunguzi wa madaktari katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ulisema pombe kali aina ya Jackie Daniels ilisababisha kifo cha mwigizaji huyo. 
Kifo cha Kanumba kiliwaumiza wengi, kwani msanii huyo alikuwa mahiri na kipenzi cha wapenzi wa filamu nchini.
Wapembuzi wa mambo wanasema huu ni msiba wa kwanza kuteka hisia za watu wengi zaidi, tangu kifo cha baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba mwaka 1999.

RIHHANA APOKEA GARI LA KIFAHARI KAMA ZAWADI YA XMAS KUTOKA KWA JAY Z...

0 comments

zawadi ya Xmas aliyopewa Rihana- a brand new Porsche 911 Turbo S Kutoka kwa rap mogul, Jay-Z akishirikiana na utawala mzima wa label ya Roc Nation.gari hii anagharama ya $200,000.

MBUNGE KABATI ATOKA NA WIMBO WA MKALI NA TOP 2O YA KABATI STAR SEARCH ...

0 comments
Mbunge wa viti maalum (CCM) Ritta Kabati akiingiza mashairi katika wimbo mpya akishirikiana na vijana chupikizi 20 wa kabati star search katika studio za Top Magic Sound zilizoko Ipogoro Iringa mjini.
Na Denis Mlowe – Iringa
Muziki wa kizazi kipya wengi wanaujua kama bongo fleva wazidi kuwavutia viongozi mbalimbali na wengine wanaimba hadi sasa kama Joseph Mbilinyi aka Sugu, Vick Kamata sasa amejitokeza mbunge mwengine wa viti maalum toka chama cha mapinduzi Ritta Kabati na kuufanya uwe gumzo katika maisha ya watanzania na nchi za jirani kitu kinachofanya watu mbalimbali kujitokeza kuupenda na wengine kuamua kuingia kwa kasi katika tasnia hii ya burudani Tanzania.
Katika kuukuza zaidi muziki huu Mbunge wa Viti maalum kupita chama cha Mapinduzi mkoani Iringa Ritta Kabati akishirikiana na wasanii chipukizi 20 wa kwanza waliotokana na shindano la kutafuta vipaji la Kabati Katiba Star Search amefanikiwa kutoka wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la 'Iringa Bila Ukimwi Inawezakana' uliofanywa katika studio za Top Magic Sound chini ya mzalishaji anayekuja kwa kasi pande za Nyanda za juu Kusini Ecko Msigwa.
Wimbo huo ni harakati za mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga kama uvutaji wa bangi, kuepukana na maambukizi ya ukimwi katika mkoa huu ambao unaongoza kwa sasa nchini Tanzania na amesema kwamba wakati anafikiria kuingiza mashairi hayo kwa kweli alikuwa katika hali ya huzini kwa jinsi vijana walivyoweza kufanya vizuri katika wimbo huo kwa lengo la kuwakomboa watanzania kupitia muziki.
Baadhi ya mashairi ya hayo ni ‘ndugu zangu watanzania nina maumivu makali sana, tumepoteza ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu dira ya maendeleo inateketea ni wakati wetu kupambana iringa bila ukimwi inawezekana’ “ kwa kweli nina uhakika wa kuwafunika vijana hawa katika wimbo huu ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa mkoa huu kwa kuwa ni mkusanyiko wa vipaji vya kweli vilivyotokana na shindano nililoandaa” alisema Kabati 
Wimbo huo unatarajia kuzinduliwa rasmi leo katika radio zote za Nyanda za Juu Kusini na kisha kusambazwa katika radio zote nchini Tanzania na amewataka wadau kuwapa nguvu vipaji hivi kwa kununua kazi za vijana kwa lengo la kuwaongeza kipato na kuondoka na maisha ya vijiweni.
@kwa hisani ya francisgodwin.blogspot.com

“NIGGAZ IN PARIS” YA JAY Z NA KANYE WEST YATAWAZWA TRIPLE PLATINUM…

0 comments
Ni mwaka tayari umekatika tangu Kanye West na Jay Z waiachie kitaani albam yao ya pamoja…”Watch The Throne”…albam ambayo mpaka hivi sasa imeshanyakuwa tuzo kibao sana…ambayo kadri muda unavyozidi kusonga ndivyo tracks ndani ya mzigo zinavyozidi kushika zaidi.
Kwa mujibu wa HHNM…”Niggaz in Paris” moja kati ya ngoma makini sana zinazopatikana kwenye albam hiyo tayari imetawazwa triple platinum baada ya kufikisha mauzo ya nakala milioni 3.
Mafanikio ya baadhi ya ngoma kutoka ndani ya albam hiyo hayajaishia hapo coz ngoma “No Church in the Wild” ambayo Frank Ocean amenyonga choras flani matata pia imetawazwa GOLD..tayari imekuwa ikitumika kwenye matangazo ya magari, movies na bidhaa zingine kibao.
“Niggaz in Paris” ni ngoma Jay Z na Kanye wanaitegemea sana kwenye kuamsha watu mara zote wanapokuwa kwenye concerts mbalimbali…na mara nyingi wamekuwa wakii-perform zaidi ya mara saba kwenye tamasha moja kutokana na maombi ya fans...


T.I AZUNGUMZIA ALIVYOM’SIGN MEEK MILL GRAND HUSTLE….NI SEHEMU YA SAFARI YA MEEK MILL KIMUZIKI….

0 comments


Kabla hajawa rapper anayefahamika sana kama ilivyo sasa chini ya Maybach Music lebel…mtu mzima Meek Mill alikuwa amesign kwa muda mfupi na Grand Hustle Records ya T.I.
Akipiga interview na Power 99 fm ya Philadelphia..bosi wa zamani wa rapper huyo na mfalme kutoka South..mtu mzima T.I amezungumzia mwanzo wa Meek Mill pale Grand Hustle.
Tip amesema bado anahisi kubeba majuto ya haja kwa kumwachia Meek Mill aondoke…lakini pamoja na hayo yote anajivunia mafaniko ya mchizi huyo kwa sasa akiwa na lebel nyingine.
“Mimi na Meek Mill tulikuwa pamoja awali Grand Hustle..kutokana na mambo ya hapa na pale yaliyokuwa yananizunguka kwa wakati ule sikuweza kufanya chochote kwa yeyote…na ndicho kilichomfanya aondoke na kwenda kwa Rozay…japo nilikuwa na mkataba naye lakini sikuona maana ya mimi kumzuia wakati sikuwa na uwezo wa ku’match na situation yake…bado nilikuwa hata nikirudi nyumbani ninakuwa mambo mengi sana ya kufanya…so kama uamuzi wa kwenda MMG ulikuwa ni uamuzi mzuri kwake sikuona namna ya kulizuia hilo”…amesema T.I
Akaongeza..”Ninafurahia mafanikio yake…kiukweli kabisa…na najisikia kama nami ningehusika kwenye mafanikio hayo ingekuwa mzuka sana…mwisho wa siku maisha ndivyo yalivyo…wakati mwingine hakitokei kile unachotaka kitokee”.