Thursday, January 03, 2013

BREAKING NEWS: DEMBA BA MCHEZAJI RASMI WA CHELSEA - NEWCASTLE WATHIBITISHA KUMUUZA ..


 

DEMBA BA amekamilisha usajili wake kwenda Chelsea - huku kocha Alan Pardew akisisitiza mshambuliaji huyo ameondoka na baraka zao.
Ba, 27, mapema leo alikuwa kwenye mazungumzo na Chelsea baada ya The Blues kukubali kulipa kiasi cha £7.5million kilichopo kwenye mkataba wa BA na Toons. 

Mshambuliaji huyo wa Senegal aliachwa katika kikosi kilichopambana na Everton usiku huu.
Na Pardew alifunguka kwa kusema mshambuliaji huyo wa zamani wa West Ham ameshakubaliana maslahi binafsi na Chelsea. 

Pardew alisema: “Uhamisho umekamilika. Anaenda Chelsea na baraka zetu. Amecheza kwa mafanikio akiwa nasi na sio kitu kibaya kuondoka, vitu vyote sasa vimekamilika na tuendelee mbele.
"Hii klabu ni kubwa kuliko mchezaji yoyote kwa hakika."

Wakati huo huo beki wa kifaransa nae leo yupo St.James Park akikamilisha taratibu za mwisho kujiunga na Newcastle. source ..shaffiidauda.blogspot.com

0 comments: