Friday, January 18, 2013

Huyu ndo msanii mpya wakike alie-sign Cash Money...YMCMB ni group linaloendelea kukuwa kila siku ,hivi sasa Birdman na Slim maboss wa kundi hilo kum-sign mshiriki wa shindano la  'America's Got Talent' Sarah Lenore katika label  yao ya Cash Money record label. 


Sarah Lenore,ni muimbaji kutoka Detroit ambaye alishiriki katika kipindi cha America's Got Talent' kinachorushwa na television ya  NBC hiki ni kipindi cha tv cha kutafuta vipaji vya waimbaji , ameshakubaliana kujiunga na YMCMB  

sarah anasema kwa miaka kadhaa amekuwa akipata nafasi yaku-sign na record labels tofauti tofauti lakini hakuwa tayari ,lakini nafasi hii alioipata anazani ni njia muafaka kutambulishwa katika music industry chini  Cash Money Records. 

Hakuna  njia nzuri ya kunitambulisha kwenye music industry zaidi ya ku-sign kwenye label kubwa ,na nafasi ya kufanya kazi na  Birdman ,Slim na team nzima ya YMCMB nifaida kubwa

Baada ya maneno hayo kutoka kwa sarah ,Birdman hakukaa kimya amemzungumzia kwa kusema, "Sarah ni star kwa kila neno ,ni mtumbuizaji wenye nguvu na anasauti nzuri   . My brother Slim na mimi tunamipango mikubwa sana juu yake ‘’amesema birdman.


0 comments: