Saturday, January 05, 2013

Tyga azungumzia uwezekano wa kufanya tena albam ya collabo na Chris Brown "Fan Of A Fan 2"

Pamoja na kuja na albam yake mpya, Tyga amezungumzia uwezekano wa kufanya project mpya na  Chris Brown "Fan Of A Fan 2".
Mwaka  2012, kabla ajaachia  187 mixtape, Tyga  alisema albam yake ya Hotel California ipo karibuni kutoka na itakuwa tayari march 2013.  Tyga amesema yeye pamoja na chris Brown wame-plan collabo project ya Fan Of A Fan 2, na amezungumzia ni kwanini anapenda kufanya kazi na Brown.
Akiwa ndani ya  Power 106 Big Boy’s Neighbourhood, the Young Money rapper amesema yeye na C-Breezy wamepanga kufanya kazi pamoja lakini solo projects zinawafanya wakose muda.  “nazani yupo nje ya nchi kwasasa ,nimezungumza nae sio muda mrefu ,tuna ngoma nyingi ,japo  nadrop albam yangu March ,nafikiria yeye pia anatengeneza vitu vipya “amesema Tyga akimzungumzia C-Breezy..
Kuhusu kwanini anapenda kufanya kazi na brown ,Tyga anasema nirahisi kufanya kazi na C-Breezy na hufanya kazi pamoja studio kwa kushirikiana.
“tunafanya vitu vyote studio pamoja ,anaweza kuja na idea za ngoma tatu mpaka nne  ndani ya dakika 30,namimi natengeneza verses kwenye ngoma hizo ,na yuko fast wakati anarecord..


Tizama interview alioifanya Tyga na Power 106’s Big Boy’s Neighbourhood..

0 comments: