Thursday, January 24, 2013

Tyga atiRiRika kuhusiana na albam yake Mpya na anavyojisikia baada ya kuwa baba….
Tyga ambaye amekwisha kutangaza tarehe rasmi ya kutoka kwa albam yake ya Hotel California March 26 ,amezungumzia pia majukumu alionayo hivi sasa baada ya kuwa baba..
Tyga  akipiga story na106 & Park amesema  amekuwa busy sana akifanya kazi zake kama sio albam basi ni mixtape ,pamoja na ku-promote viatu vyake vinavyozalishwa na Reebok, the T-Raww, na pia anamtoto wa kiume ambaye amezaliwa October mwaka jana aliempa jina la Cairo.
Rapper huyo mwenye 24 kutoka YMCMB Akizungumzia juu ya kuwa baba amesema imemfanya ayakubali maisha kwa kiasi flani na haofii majukumu yaliyoongezeka baada ya kuwa baba.
 "It’s not really a challenge. It’s actually fun ’cause I’m a young parent. At the same time, I’m still enjoying my life," amesema Tyga.
Baadhi ya celebrities wamekuwa wakificha maisha yao binafsi hususani maisha ya watoto wao ,lakini Tyga sio mmoja wao ,.kwani mwanae  Cairo tayari ana Instagram account. 
Mchek Tyga akiwa ndani ya 106 & Park..

0 comments: