Saturday, January 26, 2013

Sikukuu ya chelewesha lulu kuingia uraiani,sasa kutoka jumatatu...


Kwa mujibu habari za kuaminika zilizotolewa kupitia
millardayo.com kuwa msanii wa maigizo Elizabeth Michael a.k.a Lulu angeachia
jana ijumaa january 25, watu wengi waliisubiri kwa hamu siku hii ili waweze
kufahamu ni nini kingetokea, lakini kwa bahati mbaya jana ilikuwa ni sikuu ya
Maulid kwa hiyo mahakama haikufunguliwa hivyo kumfanya Lulu aendelee kubaki maabusu.

 
Hata hivyo dhamana iko palepale na inaaminika kuwa huenda
ikatolewa siku ya jumatatu january 28, mwaka huu kama taratibu za kimahakama
zitakuwa zimekamilika na mahakama kujiridhisha. Kwa mujibu wa taarifa za ndani
za mwanzo dhamana hiyo ilihitaji sh.million
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa
muigizaji maarufu Steven Charles Kanumba, aliyefariki April, 2012.


0 comments: