Tuesday, January 15, 2013

LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNER G HABASH WAMALIZA SALAMA SAFARI YA KUTANGAZA UTALII WA NDANI MLIMA WA KILIMANJARO

Mhifadhi mkuu wa mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo akimuongoza msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro,shoto mwa Jay dee ni mpiga picha wa JayDee,Bw Justine.


Na Dixon Busagaga .

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa
jina la Lady Jay Dee, jana alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku
sita ya kupanda mlima Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima
huo na kujionea upekee wa kivutio hicho.

Katika ziara hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini
(TANAPA), msanii huyo aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia
kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa 12
jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro
(KINAPA), Erastus Lufungulo.

Msafara wa Jay Dee ulianza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro Januari
8 na kufanikiwa kufika katika kilele chake chenye urefu wa mita 5895
kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya
kushuka mlimani, Jay Dee, alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa
kwao na wakatoa wito kwa wasanii, waandishi wa habari na watangazaji
nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu yale wanayozungumza
kuhusu hifadhi hizo.

“Ziara hii imenipa mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na
niwakumbushe tu wasanii wenzangu kuchukulia zoezi la kupanda la
kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya majukumu na wajibu wao kama
wananchi wa taifa hili,” alisema Jide.

Kwa upande wake mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote
hasa wananchi wa kawaida kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la
kukuza utalii wa ndani.

http://2.bp.blogspot.com/-Cbv26YbIsxA/UPRyVDJftmI/AAAAAAAAbF8/lw68vKjmg_I/s1600/E86A2236.JPG
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni msanii Lady Jay Dee.


0 comments: