Tuesday, January 29, 2013

Kamikaze afunguka juu ya kufanya collabo na wakali kutoka Nigeria ,pamoja na track ya utam wa chocolate kuchezWa nchini humo…Member  wa kundi la Wakacha Cyril aka kamikaze Katika harakati za kuuvisha border mziki wake amefanya collabo na wakali kutoka Nigeria ,

Akipiga sory na SwahiliInfo.blogspot.com Kamikaze amesema  fans wake wategemea kusikia kazi mpya ambayo amefanya na Bebesumtin ikiwa kama solo projEct nje ya kundi lake la wakacha ,ngoma hiyo imefanyika BLING Records Nigeria chini ya producer King,


Pia Kamikaze amefunguka kuwa amewekwa kwenye collabo kubwa ya Dj bello ambaye anafanya kazi katika Radio station kubwa nchini Nigeria CAPITAL FM,Collabo hiyo imeshirikisha wasanii mbali mbali kutoka barani Africa kama Ice Prince ambaye amepata tuzo ya msanii bora wa hip hop Africa na wengine kutoka nchi kama za Zimbabwe,South Africa ,Ghana,Nigeria na Angola..

Kuhusu ni lini ngoma hizo zitatoka na kuzisikia kamikaze amesema ngoma aliofanya na Bebesumtin ataitoa hivi karibuni na collabo aliopewa na Dj bello hajajua, ila kuna tetesi Video itafanyika South Africa..

Kamikaze amesema kwasasa  ameanza kupiga step kubwa katika muziki wake kwani track yake ya  ya utam wa chocolate inapigwa nchini Nigeria kupitia CAPITAL FM ambayo ipo ABUJA…

0 comments: