Thursday, October 18, 2012

Hawa ndo wasanii watakapanda jukwaa la Mtikisiko 2012,Makambako..

Wakati jamii ya wasanii mkoani IRINGA ikilalamikia kubaniwa kwa nyimbo zao kutopewa nafasi kwenye radio stations mbalimbali mkoani humo, wasanii kuopewa nafasi ya ku-perfom kwenye MATAMASHA makubwa au kutolipwa chochote hata wapatapo nafasi ya ku-perfom..jopo la MTIKISIKO 2012 rasmi limewatangaza wasanii watatu wanaofanya vizuri sana kwa sasa kuungana na AMINI, LINAH, MPOKI na ROMA kwenye MTIKISIKO 2012 MAKAMBAKO. Wasanii hao ni MEEDA, NAOMI na mkali MED C....
Taarifa zinasema wasanii wote hawa watasainishwa mikataba ya show moja ya mchana itakayofanyika katika uwanja wa AMANI ambapo kiingilio kitakuwa ni sh. 3000 tu na watalipwa VIZURI na kupata huduma zote sawasawa na watakazozipata wasanii toka DAR...kwenye show hiyo AMINI, LINAH na MPOKI watakinukisha mpaka moja kamili jioni...na ROMA atatokea usiku pale GREEN CITY HALL kuanzia saa mbili kamili usiku mpaka majogoo...MTIKISIKO 2012..."Ndo Vileeeeee.....!!!"

0 comments: