Wiki hii imeanza na zali zaidi ya lile la mentali
kwa mtoto ambae alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana nchini Kenya,
inaweza kuwa ni ndoto aliyoota imekuwa kweli na kama hakuwahi kuota basi Mungu
amemsapraiz na kujikuta anapata deal la uhakika la kufanya muziki chini ya lebel
kubwa duniani ya ‘Konvict Muzik’
Mtoto huyo Wilson alimsimamisha Akon jijini Nairobi
juzi wakati anaelekea kupiga show katika ukumbi wa Nairobi Carnival na akaona
kabisa kuwa hii ilikuwa ni chance ya yeye kumueleza Akon ya moyoni na sio
kumuomba mkwanja kama wafanyavyo wengine…ila ni kumuomba kujiunga na lebel ya
Konvict. Duh, unaweza kudhani mtoto huyo alikuwa mwehu eeeh…dogo alirusha mkuki
vizuri!!
Baada ya Akon kukubali kusimama tu mtoto huyo
alizitumia dakika chache kumsimulia hali mbaya ya maisha aliyonayo na jinsi
ambavyo baba yake alivyomtesa na kulazimika kulala nje, akaeleza jinsi gani
anavyoupenda muziki na hana jinsi ya kuweza kuingia studio kurekodi.
Surprisingly, Akon akaamua kumpa nafasi, akaruhusu aingizwe kwenye gari lake na
wakaelekea wote kwenye concert yake.
Hatujui nini kiliendelea kwenye gari lakini
inaonekana waliendelea kuongea kuhusu yale waliyoyaanzisha. Na haikuwa rahisi
kwa Akon kumpa nafasi kirahisirahisi tu.
Wakati anaendelea na performance yake mkali huyo
toka Senegal alimuita stejini yule dogo. Kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa kubwa
kama lile…Akon akamkabidhi dogo mic na kumwambia aperform!
Ni kama ulikuwa mtihani wa mwisho kwa dogo huyo
ambao ungemtoa lawama Akon kirahisi, dogo alifunika vibaya na kuonesha kipaji
kikubwa alichonacho.
Haikuhitaji press release ama press conference
kutangaza uamuzi…Akon alichokifanya alishika mic na kutangaza mbele ya umati wa
watu, “Wilson the newest member of the Konvict family”. Ni hivyo tu dogo
anachukua pipa kwenda kuishi ndoto zake Marekani.
Huyu ni mtoto wa kiafrika mwenye story ya mafanikio
inayofanana na ya Akon.
0 comments:
Post a Comment