Thursday, July 04, 2013

50 Cent mikononi mwa sheria kwa kumpiga Baby Mama wake...

Kwa mujibu wa habari zilizoenea kwenye mitandao hivi sasa 50 Cent anakabiliwa na mashtaka ya kumshambulia  ex-girlfriend ambaye pia amezae nae Daphne Joy. Tukio lililotokea june 23 nyumbani kwa Baby mama huyo Lake, Calif.

Mwanasheria mmoja wa jiji la L.A. ameuambia mtandao wa  TMZ 50 ameshakiwa kwa kusababisha hasara ya   $7,100 kutokana na uharibifu wa vitu vilivyo kuepo ndani ya nyuma hiyo .

Na kwa mujibu wa maofisa wa Los Angels Police Dipartiment LAPD ambao waliitwa eneo la tukio wanasema mwanamama huyo aliwaeleza ,50 akiwa na hasira alivunja mlango na kasha kumpiga na kumsababishia majeraha na kasha kumfungia chumbani ..

Taarifa za maofisa wa LAPD zimeendelea  kwa kusema Rapper huyo mwenye miaka 37 anadaiwa  kuvunja vunja furniture, TV pamoja na taa na kasha kuondoka eneo la tukio kabla police hawajafika

Kutokana na tukio hilo wafuatiliaji wa mambo wanasema huenda 50 akakabiliwa na kifungo cha miaka mi 5 jela na faini ya zaidi ya ..$45,000 ,tarehe ya kusomwa hukumu imepangwa kuwa ni July 22.

Daphne na  50 walizaa motto mmoja lakini 50 anamtoto mwingine wa kiume wa  miaka 16 alizaa na Shaniqua Tompkins,

0 comments: