Wednesday, July 17, 2013

mwanasoka nigeria matatani kwa kukwepa kulipa kodi nchini ufaransa ..


 
Beki wa kushoto raia wa Nigeria  Taiye Taiwo amepatikana na kesi ya kujibu nchini ufaransa kwa madai ya kukwepa kulipa kodi nchini humo.

Mamlaka ya mapato nchini ufaransa imesema mchezaji huyo mwenye miaka 28 ambaye alikuwa anachezea Marseilles kati ya  2005 na 2011,   alikwepa kulipa kodi ya mapato/ income taxes/ kati 2008 na 2009 na pia anadaiwa kuto kulipa kodi ya mali / property taxes/ mwaka  2011

Mamlaka hiyo imesema Taiwo ambaye kwasasa anachezea club ya uturuki Bursaspor,anadaiwa jumla ya  euro €1,025,000 lakini kupitia wakili wake anaweza kuomba kulipa kwa awamu .

Taiwo tayari ameshamtuma wakili wake ili kushugulikia swala hilo.

0 comments: