Tuesday, July 23, 2013

lyrics za ngoma mpya ya ney wa mitego ni ''hatare''


mara zote Ney wa Mitego amekuwa akizungumza vitu moja kwa moja katika ngoma zake bila kuficha ficha  utaratibu ambao anaonekana kuuendeleza katika ngoma zake baada ya kuchapisha baadhi ya mistari ya ngoma yake mpya itakayokuja ,kafanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii.''Hizi Salamu ziende kwa Madam Rita na bongo star search. 
Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?!
Namuona Walter Chilambo kapigika km zamani,
haji ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, 
acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.#966#, salam zao# my new track,
aliandika Nay Wa Mitego kupitia Instagram.
hakuishia hapo akachapisha mistari mingine kupitia Facebook

''Naongea na Liz one hey Liz one, we c mtoto wa raisi Liz one. Mwambie dingi yako Masela hawamuelewi wamakonde wa mtwara hawataki tena korosho, wanaitaka ges si mtawaua na mkong'oto?! Nani lafiki wa lowasa anifikishie salam 2015 nataka agombee uraisi nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi, ts 966.# Salam zao# my new track# coming soon.!!'''

0 comments: