Thursday, July 04, 2013

Nisher akasirishwa na kuto kukubalika ARUSHA..

ukweli uliowazi kuwa huwezi kumridhisha kila mmoja katika kitu unachokifanya,  lakini mara nyingi huwa inaaminika kuwa nyumbani ndio sehemu pekee mtu unaweza kupewa support ya bila kikwazo kitu ambacho kimekuwa tofauti kwa Nisher.

Pamoja na mafanikio ambayo ameanza kuyaona kwa muda mfupi baada ya kutengeneza video zilizokubali ikiwemo Jikubali ya Ben Pol inayoonekana Ch o...


Kupitia ukurasa wake wa facebook Nisher ameelezea hisia zake za masikitiko baada ya kugundua kuwa hakubaliki nyumbani (Arusha) na badala yake amekuwa akikubalika zaidi mikoani,  kitu ambacho kimemfurahisha  kupokelewa vizuri mikoani lakini upande mwingine ameumia  kuchukuliwa poa nyumbani alipopategemea angekubalika zaidi kabla ya mikoani.

Hii ndio status ya Nisher

“Kunakitu naomba niulize… Mi ni NISHER, sawa but nashangaa Napata upendo mwingisana kwenye Media nyingi sana nchi nzima, Dar, zanzibar, morogoro, iringa mwanza yani hakuna siku sipigiwi simu presenters wanataka interviews na mimi ila na shangaa A.T.L ambako ndo kwangu watu wachache sana ndo wanajivunia NISHER, this is SO UNBELIEVEBLE NA INANI-VUNJA-MOYO kwamba nyumbani nlitakiwa kupata Love nyingi zaidi KWASABABU NAWAKILISHA MJIWANGU but inavyoonekana wanao nihitaji na kunionyesha upendo wakweli ni walioko mikoani.. leo nikisema nihamie Huko, Mtaanza. Tulijua tu atahama. mnasahau kua Mi ni MTOTO wenu! Haaaaaya! Mi nawaangalia tu. Wanao-isifia Mvua, itawanyeshea!! Wasio ihitaji kuna baridi na jua…nisher”.

Nisher ametengenza Video ya Ben Pol ‘Jikubali’ ambayo imeanza kuonekana Channel O ya Afrika Kusini hivi karibuni,

0 comments: