Tuesday, July 09, 2013

FAHAMU mipango ya M2theP Baada ya kumpoteza Rafiki yake Albart Mangwea.

Wachezaji-wa-bongo-Fleva-wakijiandaa-kuingia-uwanjani
Baada ya kuondokewa na kipenzi chake cha karibu (Ngwea), M2thep amesema yuko mbioni kuchora tattoo kubwa yenye sura ya Ngwea mgongoni katika kumkumbuka kwake, na kwasababu alipokuwa nae South Africa mara ya mwisho alimtakia kuwa anataka kuchora tattoo.


 

"Tattoo ya chozi hii niliichora kwasababu ya kuondokewa na mama yangu mzazi, hii inaashiria nilipoondokewa na mama yangu, then niliweza kuchora tattoo hii ya chozi, yaah nikachora tattoo hii ya chozi, nikachora tattoo ya music mkononi, ambapo mi ni blood ambae napenda sana music, nikachora melody kwenye shingo,then nataka kuchora tattoo kubwa ngongoni yenye picha yake, nadhani itakuwa ndio kumbukumbu yangu kubwa, ambayo ntaichora mgongoni, kichwa kizima cha Albert nitakichora, yaani nategemea hicho kitu kukifanya, yaani ntakapo tulia nadhani, ntakapotulia ntaweza kufanya hicho kitu, kwasababu sasa hivi yenyewe ndio nimeanza ku recover, na natoka toka sasa hivi na vitu vingi vinanihusu studio nini, ila nikipata muda ndio ambacho cha muhimu, yaani hata yeye mwenyewe kwanza kipindi anakuja soth africa alisema mwenyewe anataka kuchora tatto, lakini kwa bahati mbaya mpaka anaondoka hajaweza kuchora hiyo tatto ambayo alikuwa anaitarajia yeye wenyewe kuichora, ambacho mi ndio nitakachokifanya kumuenzi, ntachora tattoo kubwa mgongoni ambayo itakuwa na picha yake" amesema M2thep

Nakuhusu kazi zake za muziki M2theP amesema

Kuna Foundation ya Chemba ambayo inamuhusu Mangwea itakayo kuwa chini yangu, nadhani kuna Danger View Music, kuna vijana ambao aliwaacha Mangwea  walio chini yangu pia. Kuna project yangu ya nyimbo inaitwa “Wasambe” ambayo itakuwa inaelezea maisha yangu na rafiki yangu wakati tupo Afrika kusini ni msemo ambao tulikuwa tunautumia sana tukiwa Afrika kusini ukiwa una maana “twende zetu ee”. Kuna ngoma nimefanya na Suma G, Mirror, Country Boy ambayo iko tayari sasa hivi nadhani kama next week nafanya video ya hiyo nyimbo amesema M2P

Foundation itakuwa inamhusu  Albert itakayokuwa chini yangu, tutakuwa tunatoa nyimbo, tunafanya nyimbo ambazo alizifanya pia na zile ambazo zipo studio tunazifanya mix tena tunawapa watu wengine wapige vocal ambayo tutatengeneza album, itakayokuwa ya foundation iliyo chini yangu  na Majani.

Kuna nyimbo ambayo nafanya na Diamond kwa P.Funk Majani, Bongo record na Jay Mo, ngoma inaitwa Mungu Ndo Anajua inayomhusu rafiki yangu kipenzi changu Albert Mangwea.

0 comments: